1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel kuwatuma walinda amani kwa umoja wa mataifa

9 Novemba 2005

Israel inafanya mazungumzo na umoja wa mataifa ili kuwatuma wanajeshi wake kama walinda amani wa umoja huo katika maeno ya vita. Maofisa wanasema hatua hiyo inafuatia kuboreka kwa mahusaiano kati ya Israel na jamii ya kimataifa.

Israel haimo katika orodha ya mataifa 117 yatakayopeleka wanajeshi wa kulinda amani katika maeneo yanayokumbwa na vita.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Israel, Mark Regev, amesema wazo la wanajeshi wa Israel kushiriki katika juhudi za kulinda amani liliwasilishwa tangu miaka ya 1990 lakini likaongezewa nguvu hivi majuzi. Regev amesema wanajeshi wa Israel walio na uzoefu wa vita katika mashariki ya kati, watafaa katika kuyatengua mabomu ya kutegwa ardhini.

Kuondoka kwa Israel kutoka ukanda wa Gaza kulipokelewa vizuri na umoja na mataifa na katibu mkuu wa umoja huo, Kofi Annan, alifutilia mbali ziara yake nchini Iran wakati rais wa nchi hiyo, Mahmoud Ahmadinejad, alipotaka Israel ifutwe kutoka ramani ya dunia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW