JERUSALEM: Israel yalaumiwa.
25 Machi 2005Matangazo
Mkuu wa maswala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya bwana Javier Solana, ameulaumu mpango wa Israel wa kutaka kupanua makaazi katika Ukingo wa Magharibi.
Bwana Solana ametaka waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon asimamishe mpango huo.
Agizo hilo limetolewa baada ya Israel kutoa kibali cha ujenzi katika mji wa Maale Adumin ulio Mashariki ya jerusalem.
Bwana Solana amekilaani kitendo hicho na kusema kuwa kimekiuka mkataba mpya wa amani wa Mashariki ya Kati ulioandaliwa na Marekani, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Urusi.