JERUSALEM: Israel yatoa pesa za ushuru za Wapalestina
19 Januari 2007Matangazo
Israel imetoa kiasi cha Dola milioni mia moja rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina.Saeb Erekat,msaidizi mkuu wa Abbas amesema pesa hizo zitagawanywa miongoni mwa mashirika binafsi na vile vile zitatumiwa kwa huduma za kiutu.Israel kwa jumla imezuia zaidi ya Dola milioni mia 5 ambazo ni ushuru wa forodha uliokusanywa na Israel kwa niaba ya Wapalestina.Israel ilizuia kutoa pesa hizo baada ya chama cha Hamas kushika madaraka kufuatia ushindi wa uchaguzi wa Januari mwaka 2006.Israel,Marekani na Umoja wa Ulaya zinakitazama chama cha Hamas kama ni kundi la kigaidi.