1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Jumba la makumbusho lafunguliwa.

16 Machi 2005

Wawakilishi wa mataifa zaidi ya 40 wameshiriki katika kuzinduliwa jumba jipya la makumbusho la JAD VACHEM la wahanga wa mauaji ya mafashisti mjini Jerusalem.

Rais wa Israel Mosche Katsav amewaongoza watu mashuhuri katika kumbukumbu hizo miongoni mwao akiwemo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Joschka Fischer na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Koffie Annan.

Waliosalimika na mauwaji hayo ya manazi katika vita vikuu vya pili vya dunia pia walialikwa katika kumbukumbu hizo.

Waziri mambo ya nchi za nje wa Israel Silwan Schalom amemtaja waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani kuwa ni rafiki wa Israel.

Amesifu pia juhudi zinazo endeshwa na mwana diplomasia huyo wa Ujerumani.

Jumba hilo la makumbusho lilojengwa baada ya miaka kumi la YAD VACHEM limefunguliwa wakati mmoja na maadhimisho ya mika 60 tangu vita vikuu vya pili vya dunia vilipomalizika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW