1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM. Kamanda apoteza kazi kwa utovu wa nidhamu wa kikosi chake.

27 Mei 2005

Kamanda wa kikosi cha wanajeshi wa Israel walioingia kwa lazima kwenye nyumba ya familia ya Kipalestina katika ukingo wa magharibi kwa madai kuwa wakitaka kuangalia fainali ya mchuano wa mechi ya mpira wa miguu amesimamishwa kazi kufuatia kisa hicho.

Habari hizo zilionyeshwa katika televisheni ya Israel na kuonyesha uharibifu mkubwa wa mali katika nyumba hiyo.

Jeshi la Israel limekiri kuwa wanajeshi wake waliingia katika makao hayo lakini limekana kuuhusika na uharibifu uliofanyika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW