1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Kiongozi wa Hamas amekamatwa

10 Aprili 2005

Polisi nchini Israel wamemkamata kiongozi wa wanamgambo wa Kipalestina aliyeingia mji wa Jerusalem kinyume na sheria,akitaka kuhudhuria maandamano kwenye eneo lililo takatifu kwa Waislamu na Wayahudi.Kiongozi wa Hamas,Sheikh Hassan Yussef,aliachiliwa huru hivi karibuni tu kutoka jela ya Israel.Hapo mapema kwa mamia polisi wa Kiisraeli mjini Jerusalem,walilizingira eneo takatifu la Waislamu Haram al-Sharif ambalo pia ni takatifu kwa Wayahudi na huitwa Temple Mount.Hatua hiyo ilichukuliwa ili kuzuia maandamano ya kikundi cha Wayahudi wenye siasa kali za bawa la kulia katika eneo hilo.Wafuasi wengi wa kikundi chenye siasa za kulia cha Revava walitiwa ndani.Kikundi hicho kinaupinga mpango wa waziri mkuu Ariel Sharon kutaka kuondoka kutoka Ukanda wa Gaza na miji minne kwenye Ukingo wa Magharibi.Kwa upande mwingine wanamgambo wa Kipalestina wametishia kujitenga na mapatano ya kusitisha mapigano yaliokubaliwa pamoja na Israel,ikiwa maandamano yatafanywa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW