1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem Majeshi ya Israel yauwa wanne.

24 Septemba 2005

Majeshi ya Israel yamefanya mashambulio zaidi ya ndege za kivita katika eneo la kaskazini ya ukanda wa Gaza.

Jeshi limesema mashambulio hayo yamelenga katika eneo la wazi ambako wapiganaji wa Kipalestina wamekuwa wakirusha makombora yao.

Kiasi cha Wapalestina wanne wameuwawa leo katika mashambulio hayo ya Israel katika wilaya ya mashariki ya mji wa Gaza, duru za hospitali zimesema.

Watu walioshuhudia wamesema kuwa wawili kati ya wale waliouwawa walikuwa wanachama wa tawi la kijeshi la kundi la Hamas ambao walikuwa wakisafiri katika magari mawili wakati helikopta ilipoyashambulia magari hayo kwa makombora.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW