1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Mapambano yazidi kupamba moto Lebanon.

2 Agosti 2006

Israel imefanya mashambulizi makubwa ya aridhini dhani ya Lebanon .

Makomandoo wa Israel wamevamia hospitali moja inayoendeshwa na Hizbollah katika mji wa kaskazini mashariki wa Baalbek.

Mji huo uko kilometa 130 kaskazini ya mpaka wa kaskazini wa Lebanon na Israel.

Wamewakamata wapiganaji kadha wakati wa operesheni iliyofanywa na majeshi ya anga na kuwachukua hadi ndani ya Israel.

Wakati huo huo , makamu wa waziri mkuu wa Israel Shimon Peres amesema kuwa inaweza kuchukua wiki kadha kwa Israel kumaliza kabisa kitisho kinacholetwa na wapiganaji wa Hizbollah.

Lakini pia amesema kuwa majeshi ya Israel yameharibu asilimia 70 hadi 80 ya makombora ya masafa marefu ya Hizbollah na majeshi hayo yako karibu na kulipatia kundi hilo la Kiislamu pigo kubwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW