JERUSALEM: Marekani kurejesha uhusiano wa kawaida na Palestina
18 Juni 2007Balozi wa Marekani mjini Jerusalem, Jacob Wales, amesema leo kwamba Marekani itarudisha uhusiano wa kawaida na serikali mpya ya Palestina.
Katika mkutano wake na waandishi habari mjini Jerusalem baada ya kukutana na waziri mkuu mpya wa serikali ya mamlaka ya Palestina, Salam Fayyad, balozi Wales amesema Marekani inamuunga mkono kiongozi huyo na serikali mjini Washington itatoa taarifa kamili kuhusu mpango wake wa kuisadia sderikali mpya ya Palestina.
Viongozi hao walizungumzia pia kuhusu hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza na njia za kuhakikisha raia hawateseki.
Wakati huo huo, msemaji wa rais Abbas, Nabil Abu Rudeina amesema rais George W Bush wa Marekani leo amezungumza kwa njia ya simu na rais Mahmoud Abbas na kumhakikishia atamuunga mkono licha ya kundi la Hamas kulidhibiti eneo la Ukanda wa Gaza.