1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Mashambulio ya Israel yataendelea

28 Julai 2006

Serikali ya Israel imetangaza kuwa itaendelea na mashambulio yake ya kijeshi dhidi ya vituo vya Hezbollah nchini Lebanon.Waziri wa ulinzi wa Israel,Amir Peretz alipozungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari mjini Jerusalem alisema,shabaha ya mwisho ni kuunda eneo maalum la usalama kulinda mpaka wa Israel kaskazini mwa nchi.Wakati huo huo baraza la usalama la Israel limeamua kutopanua mashambulio yanayofanywa na majeshi yake ya ardhi kavu.Lakini wanajeshi wa akiba waliojiandikisha,wameitwa kwenda kazini. Waziri wa afya wa Lebanon amesema mashambulio ya angani yaliyofanywa na Israel yameua si chini ya watu 600.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW