1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM. mkutano katika mji mtakatifu

21 Juni 2005

Waziri mkuu wa Israel bwana Ariel Sharon leo anakutana na kiongozi wa mamlaka ya Palestina bwana Mahmoud Abbas mjini Jerusalem.Huo utakuwa mkutano wa kwanza baina ya waziri mkuu wa Israel na kiongozi wa wapalestina katika mji huo mtakatifu ambao ni tufaa la mgogoro wa mashariki ya kati.

Kila upande unadai Jerusalem kuwa mji wake mkuu.

Waziri mkuu wa Israel bwana Sharon anataka mkutano huo uzingatie hatua za kuwazuia wapalestina wenye siasa kali kuvuruga mpango wa Israel wa kuondoka ukanda wa Gaza unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwezi wa agosti.

Israel inadai kwamba bwana Mahmoud Abbas hajachukuwa hatua za kutosha katika hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW