1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM. Netanyahu atoa hakikisho la kumpinga Ariel Sharon

31 Agosti 2005

Waziri mkuu wa zamani wa Israel Benjamin Netanyahu ametangaza nia yake ya kutaka kumpinga waziri mkuu Ariel Sharon katika kugombea uongozi wa chama cha Likud.

Tangazo hilo limejitokeza muda mchache tu baada ya Benjamin Netanyahu kujiuzulu wadhfa wake kama waziri wa fedha wa Israel kusisitiza hatua yake ya kupinga mpango wa Ariel Sharon wa kuwahamisha ,masetla wa kiyahudi kutoka Ukanda wa Gaza na sehemu za Ukingo wa Magharibi.

Lakini mbali na matukio yote hayo mpango wa Ariel Sharon unaungwa mkono na raia wengi wa Israel hata ingawa wengi wa wajumbe wa Likud waliupinga mswaada huo katika kura bungeni.

Kamati kuu ya chama cha Likud inatarajiwa kukutana mwezi septemba ili kupitisha tarehe 22 Novemba kuwa ndio siku ya kupiga kura ya awali ya kumchagua kiongozi wa chama hicho.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW