1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Rice akatazwa kwenda Beirut

30 Julai 2006

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amethibitisha kwamba hatokwenda mjini Beirut kufuatia mauaji ya walebanon katika mji wa Qana. Rice alikuwa amepangiwa kukutana na viongozi wa Lebanon lakini maofisa wa nchi hiyo wakamuomba asiende kufuatia shambulio dhidi ya mji wa Qana.

Maofisa wa serikali ya Lebanon wamefanya mkutano wa dharura na kuamua wasimkaribishe Condoleezze Rice nchi mwao na kuzuia mazumguzo yoyote ya hivi karibuni yanayolenga kumaliza mapigano.

Rais wa Lebanon Emile Lahhoud amesema Marekani inabeba dhamana kwa kile alichokiita mauaji ya halaiki ya walebanon mjini Qana.

Condoleezza Rice yumo mjini Jerusalem kukutana na viongozi wa Israel. Anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Israel, Tzipi Livni na waziri wa ulinzi Amir Perez.

Vyombo vya habari nchini Israel vimeripoti kwamba Condoleezza Rice atajadili kanuni za kusitishwa mapigano na kupelekwa kwa kikosi cha kimataifa kusini mwa Lebanon, kitakacholisaidia jeshi la Lebanon.

Waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert amesema hakuna uwezekano wowote wa Israel kukubali pendekezo la kusitisha mapigano kwa wakati huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW