JERUSALEM : Rice akutana na Sharon
22 Julai 2005Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condooleza Rice amekutana na Waziri Mkuu wa Israel Ariel Sharon leo hii katika mwanzo wa jitihada mpya za kidiplomasia kuhakikisha kufanikiwa kujiondowa kwa Israel kutoka Ukanda wa Gaza hapo mwezi ujao.
Mkutano huo kwenye shamba la Sharon katika jangwa la kusini la Negev unafanyika bila ya kuvishirikisha vyombo vya habari na hakuna mkutano uliopangwa kufanyika na waandishi wa habari.
Rice ambaye amewasili Israel hapo jana pia anatazamiwa kukutana na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas katika mji wa Ukingo wa Magharibi wa Ramallah hapo kesho.
Mpango huo wa Israel kujitowa Gaza umekabiliwa na upinzani wa maelfu ya waandamanaji na walowezi wengi wa Kiyahudi wameapa kutoziwacha nyumba zao zilioko katika eneo hilo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel.