JERUSALEM: Rice amekutana na Olmert
30 Julai 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani,Condoleezza Rice amekutana na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert mjini Jerusalem kujaribu kupata msingi wa kuanzisha majadiliano ya kumaliza mapigano nchini Lebanon.Mada muhimu katika mazungumzo yao ni suala la kupeleka vikosi vya kimataifa kulinda usalama kusini mwa Lebanon.Waziri mkuu wa Uingereza,Tony Blair katika mahojiano yake na BBC amesema huenda makubaliano yakapatikana katika siku chache zijazo.Kwa upande mwingine rais Jacques Chirac wa Ufaransa alipozungumza na Blair na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan kwa njia ya simu,ametoa mwito wa kusitisha mapigano.
