JERUSALEM: Rice azungumzia taifa la Palestina
14 Novemba 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bibi Condoleezza Rice akiendelea na ziara yake ya Mashariki ya Kati amezungumzia suala la kuundwa taifa la Palestina.Lakini kwanza wakuu wa Kipalestina lazima wayadhibiti makundi ya wanamgambo aliongezea Dr.Rice.Lengo la majadiliano yake hii leo pamoja na waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas katika miji ya Jerusalem na Ramallah ni kufufua majadiliano ya amani ya Mashariki ya Kati yaliyokwama.