1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Rice ziarani Mashariki ya Kati

19 Juni 2005

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Condoleezza Rice amezitaka Israeli na Palestina zishirikiane kuhusika na mpango wa Waisraeli kutaka kuondoka Ukanda wa Gaza.Amesema ushirikiano wa aina hiyo ni muhimu sana.Rice alizungumza na waandishi wa habari,baada ya kukutana na rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina mwanzoni mwa ziara yake ya Mashariki ya Kati yenye nia ya kupiga jeki utaratibu wa amani.Leo jumapili,Rice anakutana na waziri mkuu wa Israel,Ariel Sharon,ikitarajiwa kuwa Rice ataitaka Israel isitishe ujenzi wa makazi mapya ya walowezi wa Kiyahudi.Wakati wa ziara yake ya Mashariki ya Kati,Rice atakwenda pia Jordan,Misri na Saudi Arabia kabla ya kuhudhuria mikutano ya kimataifa mjini Brussels na London.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW