JERUSALEM: Sharon atishia kuchukua hatua kali
25 Julai 2005Matangazo
Waziri Mkuu wa Israel,Ariel Sharon ametishia kuchukua hatua kali kujibu vifo vya Waisraeli wawili vilivyosababishwa na Wapalestina wenye bunduki kwenye mpaka wa Gaza siku ya Jumapili.Vikosi vya Israel vimesema vimewapiga risasi na kuwauwa watu wawili wenye bunduki waliohusika na mauaji ya Waisraeli hao wawili.Makundi matatu mbali mbali ya wanamgambo wa Kipalestina……Islamic Jihad,al Aqsa Martyrs Brigade na Popular Resistance Committees,yote yamedai kuwa ndio yamehusika na shambulio la Jumapili.Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas amelilaani shambulio hilo,lililotokea mwishoni mwa ziara ya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Bibi Condoleezza Rice katika eneo hilo.