1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Sharon katika hali mbaya zaidi

24 Julai 2006

Madaktari wanaomtibu aliekuwa waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon wemesema kwamba hali yake imezidi kuwa mbaya lakini hayupo karibu na hatari ya kufa.

Msemaji wa hospitali amearifu kuwa bwana Sharon anakabiliwa na matatizo ya mafigo na kwamba yametokea mabadiliko katika ubongo wake. Hatahivyo madaktari hawajaona haja ya kumfanyia chochote kwa sasa.

Bwana Sharon alipoteza fahamu mnamo mwezi januari, na tokea wakati huo hajazinduka.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW