1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Sharon kukutana na Abbas wiki ijayo

6 Oktoba 2005

Waziri Mkuu wa Israel Ariel Sharon na Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas wanapanga kukutana wiki ijayo.

Msemaji wa Mfalme Abdullah wa Jordan amesema viongozi hao wawili watakutana Ijumaane ijayo lakini hakutaja mahala watakapokutana.Maafisa wa Israel na Palestina wamethibitisha kwamba viongozi hao wanapanga kukutana lakini wamesema tarehe na mahala pa kukutana kwa ajili ya mazungumzo hayo kutaamuliwa wakati wa mazungumzo kati ya washauri yatakayofanyika hapo kesho.

Mkutano wao wa viongozi uliokuwa umepangwa kufanyika Jumapili iliopita ulifutwa baada ya kuzuka kwa machafuko ya umwagaji damu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW