JERUSALEM: Sharon na Abbas kukutana karibuni
23 Aprili 2005Matangazo
Waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon na Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas wamekubali kukutana hivi karibuni kuujadili utaratibu wa amani.Lakini msemaji wa Sharon amesema hakuna tarehe maalum iliyopangwa kwa mkutano huo.Abbas na Sharon walikutana kwa mara ya mwisho mwezi wa Februari nchini Misri.Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya pande zote mbili yalitangazwa kwenye mkutano huo wa kilele.Kwa upande mwingine,duru za serikali ya Wapalestina zimedokeza kuwa Rais Abbas huenda akawateua viongozi wapya kuchukua nafasi za wakuu wa hivi sasa kuhusika na huduma za usalama.Hatua hiyo itatimiza dai kuu lililotolewa na Israel na Marekani.
