JERUSALEM: Sharon na Abbas kukutana mwezi huu
4 Juni 2005Matangazo
Ofisi ya waziri mkuu wa Israel imesema kuwa Ariel Sharon atakutana na rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas mjini Jerusalem baadae mwezi huu.Huo utakuwa mkutano wa mwanzo kati ya kiongozi wa Israel na wa Palestina katika mji ambao ni kiini cha mgogoro wa Mashariki ya Kati.Muendesha mkuu wa majadiliano ya amani upande wa Wapalestina,Saeb Erekat hakuweza kuthibitisha mahala pa mkutano lakini alisema utafanywa katika eneo hilo.