1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Sharon na Abbas kukutana New York

5 Septemba 2005

Waziri mkuu wa Israel,Ariel Sharon na kiongozi wa Wapalestina,Mahmoud Abbas wanatazamiwa kukutana mwishoni mwa mwezi huu mjini New York.Gazeti la Kiisraeli,Haaretz limesema viongozi hao wawili watakutana pembezoni mwa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.Hapo awali Abbas alisema majadiliano ya amani kuhusu Mashariki ya Kati yanapaswa kuanzishwa mara tu ya Israel kumaliza kuhama kutoka Gaza,ikitarajiwa kuwa utaratibu huo utakamilishwa kati kati ya mwezi Septemba.Katika mahojiano yake na Shirika la habari la AP,Abbas alisema ni matarajio yake kuwa hadi mwakani kutaundwa taifa la Palestina.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW