JERUSALEM: Steinmeier akutana na Livni
10 Agosti 2006Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, amesema Israel inautaka Umoja wa Mataifa upitishe azimio juu ya mgogoro wa Mashariki ya Kati haraka iwezekanavyo.
Steinmeier ameyasema hayo baada ya kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Israel, Tzipi Livni, mjini Jerusalem. Amewaambia waandishi habari kwamba haijabainika wazi ni lini azimio la Umoja wa Mataifa la kusitisha mapigano litakapopitishwa.
Kiongozi huyo amezihimiza Israel na Lebanon kutumia juhudi za kisiasa kuumaliza mzozo wa Mashariki ya Kati.
Stenmeier amesema haijulikani mazungumzo ya mjini New York yatamalizika lini, lakini akasema yapo matumaini ya kufikia makubaliano hivi karibuni.
Matamashi haya yanatofautiana na ya waziri wa ulinzi wa Israel, Amir Peretz, aliyesema azimio huenda lipitishwe kufikia mwishoni mwa juma.
Waziri Steinmeier amepangiwa kukutana na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert.