JERUSALEM: Steinmeier ziarani Mashariki ya Kati
9 Agosti 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amekutana na waziri wa ulinzi wa Israel,Amir Peretz mjini Jerusalem.Steinmeier anakutana pia na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na waziri mwenzake wa kigeni Zippi Livni, kujadili njia ya kuumaliza mgogoro wa Lebanon. Siku ya Jumanne alipokutana na waziri mkuu wa Lebanon Fuad Siniora,waziri Steinmeier alisema pendekezo la Beirut kuwa ipeleke kikosi chake cha wanajeshi 15,000 kusini mwa Lebanon,huenda likaiimarisha serikali ya Lebanon.
