JERUSALEM : Steinmeir azuru Israel
10 Agosti 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir amesema anaona kuna fursa ya kufikiwa kwa suluhisho la kidiplomasia katika mzozo kati ya Israel na Hezbollah.
Baada ya mazungumzo mjini Jerusalem na Waziri Mkuu Ehud Olmert hapo jana Steinmeir amesema usitishaji wa mapigano unaweza kufikiwa chini ya msingi wa azimio la Umoja wa Mataifa ambalo hivi sasa linashughulikiwa na Baraza la Usalama.
Steinmeir pia ameelezea wasi wasi mkubwa juu ya hali ya maafa ya kibinaadamu nchini Lebanon.
Awali Steinmeir alikuwako mjini Beirut ambapo alikutana na viongozi wa Lebanon.