1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Vikosi vya Israel vyasonga ndani ya Lebanon

10 Agosti 2006

Vikosi vya Israel vimeingia kilomita 10 kusini mwa Lebanon mapema leo, ili kuzuia maroketi ya Hezbollah yanayovurumishwa kutoka mji wa al Khaim. Walioshuhudia wanasema wanajeshi hao wamekifikia kijiji cha Dibeen.

Maofisa wa jeshi wamekanusha madai kwamba hatua hiyo inafuatia idhini iliyotolewa na baraza la usalama la Israel hapo jana ya kupanua operesheni.

Uamuzi huo ulipitishwa baada ya jeshi la Israel kuthibitisha kwamba wanajeshi wake 15 waliuwawa katika mapigano makali na wanamgambo wa kundi la Hezbollah.

Hiyo ni idadi kubwa zaidi ya wanajeshi wa Israel kuuwawa katika siku moja tangu vita kati ya Israel na Hezbollah vilipoanza. Wanajeshi wengine 38 walijeruhiwa wakiwemo wanajeshi wa akiba.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani nchini Marekani, Sean McCormark, amesema Israel ina haki ya kujilinda kutokana na mashambulio ya Hezbollah lakini serikali ya Washington ina wasiwasi juu ya hali ya kibinadamu na imeitaka Israel iwe na uangalifu mkubwa ili kuzuia vifo vya raia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW