1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Walowezi waanza kuhama

16 Agosti 2005

Katika utekelezaji wa mpango wa kuondoka ukanda wa Gaza, serikali ya Israel imeshaondoa makaazi matano ya walowezi wa kiyahudi katika ukanda wa Gaza.

Walowezi wote wamepewa muda wa hadi kesho kuyahama makaazi yao kwa hiari, la sivyo serikali itatumia nguvu kuwahamisha. Upinzani mkali unatarijiwa kutoka kwa wa israeli wenye siasa kali, wapatao alfu tano wanaosakini katika ukanda wa Gaza kinyume cha sheria.

Habari zaidi zinasema kwamba watu mia tano wanaopinga mpango wa serikali wa kuondoka ukanda wa Gaza na ukingo wa magharibi wametiwa ndani kusini mwa Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW