1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Wanachama wa Islamic Jihad wauawa

25 Agosti 2005

Wanajeshi wa Kiisraeli wamewauwa si chini ya Wapalestina 3 walipoishambulia kwa ghafla kambi ya wakimbizi ya Tulkarem,kwenye Ukingo wa Magharibi.Maafisa wa kijeshi wa Israeli,wamesema wanajeshi walichukua hatua hiyo baada ya risasi kufyetuliwa kutoka nyumba waliyoizingira.Kwa mujibu wa wakaazi wa eneo hilo,wapangaji wa nyumba hiyo walikuwa wanachama wa kikundi cha wanamgambo wa Kipalestina cha Islamic Jihad.Hapo awali mjini Jerusalem,Mpalestina mmoja alimpiga kisu na kumuuwa Myahudi mwenye itikadi kali na alimjeruhi mwengine.Hakuna alietangaza kuhusika na shambulio hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW