1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Wanamgambo waahidi utulivu

18 Machi 2005

Waziri Mkuu wa Israel Ariel Sharon amekaribisha tangazo la kuleta utulivu la makundi ya wanamgambo wa Kipalestina ambayo yamekuwa yakikutana mjini Cairo Misri.

Hata hivyo amemtaka Rais Mahmoud Abbas wa Palestina kuhakikisha kwamba hatimae makundi hayo ya wanamgambo yanapokonywa silaha.Makundi hayo 13 hayakutaja neno usitishaji mapigano kwenye tangazo lao lakini yamekubaliana kusitisha kwa masharti mashambulizi dhidi ya Israel.Yamesema kuendeleza usitishaji wa mapigano kutategemea iwapo Israel itawaachilia huru wafungwa zaidi wa Kipalestina pamoja na kujiepusha kufanya mashambulizi kwenye maeneo inayoyakalia kwa mabavu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW