1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM

16 Februari 2005

Waziri Mkuu wa Israel,Ariel Sharon amesema ataendelea kusonga mbele na mpango wake wa kuondoka kutoka maeneo ya Ukanda wa Gaza,licha ya vitisho vya kumuua vinavyotolewa na Wayahudi wenye msimamo mkali wanaopinga mpango wake huo.

Bwana Sharon pia amewaambia waandishi wa habari mjini Jerusalem,kuwa Israel imeanza kushirikiana na Mamlaka ya Wapalestina katika mpango wake huo.

Amesema amedhamiria kuhakikisha kuwa suala la kuondoka kwa vikosi vya Israel pamoja walowezi wa kiyahudi,hakutatoa mwanya kwa vikundi vya wanamgambo wa Kiislamu kuchukua nafasi yao.

Mpango huo wa kuondoka katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa na Israel,awali ulikuwa unahusu upande mmoja tu.

Wakati huo huo Wabunge wa Israel wameanza kuujadili muswada uliosomwa mara ya pili,ambao utatoa ufafanuzi wa namna watakavyofidiwa Wayahudi 8,000 watakaohamishwa kutoka Gaza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW