JERUSALEM
15 Februari 2005Matangazo
Serikali ya Israel imetangaza mipango ya kujenga makazi mapya ya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo wanayoyashikilia ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi kwa ajili ya familia 500 za walowezi ambao wamelazimishwa kuhama Ukanda wa Gaza.Bunge la Israel linajadiliana juu ya malipo ya fidia kwa walowezi zaidi ya 8,000 ambao wanaondoshwa kutoka Gaza.
Wakati huo huo Waisrael na Wapalestina wamekubaliana kukabidhiana kazi za kulinda usalama kwa Wapalestina katika baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi.Waziri mmoja wa Wapalestina anayeshughulika na masuala ya upatanishi,amesema katika kutekeleza mpango huo,jeshi la Israel kwanza litaondoka kutoka mji wa Jericho pamoja na maeneo yanayozunguka mji huo.