JERUSALEM:Israel kuondoka haraka kusini mwa Lebanon
16 Agosti 2006Matangazo
Kamanda wa majeshi ya Israel amesema majeshi yake yanaweza kukamilisha hatua ya kuondoka kusini mwa Lebanon mnamo kipindi cha siku 10.
Kamanda huyo jenerali Dan Halutz ameiambia radio ya kijeshi ya Israel kuwa hatua hiyo inaweza kukamilishwa ikiwa hali itakuwa tulivu. Amesema majeshi yake yanaweza kuondoka kwenye sehemu zinazotarajiwa kuwa chini ya udhibiti wa majeshi ya Lebanon na ya Umoja wa Mataifa.
Wakati huo huo habari zinasema kuwa mapatano ya kuacha mapigano yanaendelea kutekelezwa nchini Lebanon licha ya matukio ya hapa na pale kusini mwa Lebanon.