1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Israel yaibebeduwa Marekani

3 Desemba 2003
Israel hapo jana imeibebeduwa Marekani rafiki yake wa karibu kwa kusema kwamba waziri wa mambo ya nje wa Marekani Colin Powell atafanya kosa iwapo atakutana na waasisi wa mpango wa amani wa ishara kwa Mashariki ya Kati. Powell alijibu katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Tunis kwamba ana haki ya kukutana na yoyote yule mwenye fikra za kukomesha mzozo kati ya Israel na Wapalestina. Baadae alipokuwa katika ndege akielekea katika mji wa Marakesh nchini Morroco Powell amewaambia waandishi wa habari kwamba anataraji kukutana na waasisi wa mpango huo wa amani usio ramsi unaojulikana kama Makubalino ya Geneva yumkini siku ya Ijumaa. Wakati akianza ziara yake ya Afrika Kaskazini nchini Tunisia Powell amezitaka Algeria na Morroco kuanza mazungumzo moja kwa moja kati ya nchi hizo kutatuwa mzozo wa Sahara Magharibi ambao umetia sumu uhusiano kati ya majirai hao wa Afrika Kaskazini kwa zaidi ya miaka 20 sasa. Morroco imekuwa ikitaka kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Algeria kwa kusema kwamba mzozo juu ya koloni hilo la zamani la Uhispania ni kati ya nchi hizo mbili.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW