1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Israel yaionya Syria

7 Januari 2004
Mkuu wa majeshi wa Israel amedokeza leo hii kwamba Syria yumkini ikakabiliwa na mashambulizi zaidi ya anga kama yale yaliofanywa hapo mwezi wa Oktoba iwapo itashindwa kuwadhibiti wanamgambo wa Kipalestina ndani ya mipaka yake.
Luteni Generali Moshe Yaalon ametowa onyo hilo katika matangazo ya radio ya kijeshi na linakuja wakati Israel imedokeza kwamba inaangalia iwapo kweli Rais Basher al Assad wa Syria ana utashi wa kuanza tena mazungumzo ya amani.
Hapo Oktoba tano Israel ilishambulia kile ilichokiita kambi ya mafunzo ya wanamgambo ndani kabisa ya ardhi ya Syria baada ya mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha wa Kipalestina kuuwa watu 23 kwenye mkahawa katika mji wa Haifa nchini Israel.
Habari kutoka mji wa Nablus zinasema wanajeshi wa Israel leo wamewauwa Wapalestina watatu katika msako wa wanamgambo katika Ukingo wa Magharibi na kuzusha mayowe makali ya hasira katika maziko kwa kushutumiwa sio tu Israel bali pia viongozi wa Palestina kwa kushindwa uongozi.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW