1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM:Mapigano makali bado yanaendelea Kusini mwa Lebanon

20 Julai 2006

Mapambano yanaendelea kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon.Israel imesema kwamba inaamini hadi sasa imeweza kuharibu asilimia 50 ya nyenzo za kijeshi za Hezbollah.

Waziri wa usafiri ambaye zamani alikuwa waziri wa Ulinzi Shaul Mofaz amenukuliwa akisema jeshi la Israel lazima liruhusiwe kukamilisha opresheni yake nchini Lebanon.

Kufuatia kuongezeka kwa mashambulio huko kusini mwa nchi ya Lebanon waziri mkuu Fuoad Siniora ametoa wito akisema….

’’Kwa niaba ya walebanon kutoka mjini Beirut hadi Baalbak ,Nablus,Tieri,Saidon hadi kaanan na kwa kila mmoja katika vijiji 21 vilivyoko kusini ambako kumetangazwa kuwa eneo la hatari na Israel,nawaomba muachane na mapigano bila ya kutia walakini wowote na wanamgambo wa Hezbollah ninawaomba muwaachilie mateka wanajeshi wa Israel.’’

Kwa mujibu wa radio ya Israel waziri Mofaz amesema wito uliotolewa na Hezbollah kwa serikali ya Iran wa kuomba usaidizi ni ushahidi wazi kuwa kundi hilo liko kwenye matatizo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW