JERUSALEM:Olmert kuwekwa katika kitimoto juu ya vita vya Lebanon mwaka jana
29 Aprili 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Isreal bwana Ehud Olmert amesema kuwa hana nia ya kujiuzulu kutokana na lawama juu ya jinsi serikali yake ilivyoendesha vita vya nchini Lebanon mwaka jana.
Msemaji wa waziri mkuu huyo ameeleza hayo kabla ya kuchapishwa hapo kesho, ripoti juu ya makosa yaliyotendeka katika kuongoza vita hivyo.
Ripoti hiyo inatarijiwa kushutumu hatua za pupa zilizochukuliwa na serikali ya waziri mkuu Olmert baada ya wapiganaji wa Hezbollah kufanya mashambulio na kuwateka nyara askari wawili wa Israel.