JERUSALEM:Shimon Peres achaguliwa rais wa Israel
13 Juni 2007Matangazo
Mwanasiasa mkongwe wa Israel Shimon Peres amechaguliwa kuwa rais mpya wa taifa hilo baada ya kujizolea kura 86 za wabunge 120
Peres amepata ushindi katika duru ya pili ya uchaguzi kufuatia kujiondoa kwenye kinyanga’nyiro hicho wapinzani wake wawili.
Punde tu baada ya kutangazwa mshindi Peres alizungumzia suala la amani na wapalestina akisema.
Kila mmoja anachagua kiongozi wake wapalestina wanachagua viongozi wao na waisrael vile vile lakini hakuna anaweza kuishi bila amani kwa hivyo inabidi tukae na tujadiliane.
Peres mwenye umri wa miaka 83 anachukua wadhifa war ais unaoshikiliwa na Moshe Katsav ambaye anakabiliwa na kashfa ya kumbaka mwanamke.