JERUSALEM.Waziri wa mamlaka ya Palestina aachiliwa huru
30 Novemba 2006Matangazo
Mahakama ya kijesi ya Israel imemuachilia huru waziri wa chama cha Hamas kinachotawala mamlaka ya Palestina.
Mawakili wa waziri huyo wa nyumba na ujenzi wa mamlaka ya Palestina Abdul Rahman Zeidan wamesema kwamba jaji wa mahakama ya kijeshi alitoa uamuzi wa kumuachilia baada ya waziri huyo kukaa kizuizini kwa muda wa mwezi mmoja,kwa kuwa upande wa mashtaka haukuwa na ushahidi dhidi ya tuhuma zilizomkabili bwana Zeidan.
Alikabiliwa na tuhuma za kuhusika na harakati za wapiganaji wenye msimamo mkali.
Israel bado inawashikilia mawaziri wengine wanne na wabunge kadhaa wa chama cha Hamas kinachotawala mamlaka ya Palestina.