1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la anga la Israel limejipenyeza mashariki ya Libnan licha ya makubaliano ya kuweka chini silaha

19 Agosti 2006

Ndege za kivita za Israel na zile za upelelezi zimeizunguka anga ya mashariki ya Libnan.Msemaji wa jeshi la Libnan amesema ndege hizo hizo zilizopita karibu na bonde la Bakaa zilitumuliwa baadae na wanamgambo wa Hisbollah.Kuna walaiokufa toka pande zote mbili.Kabla ya hapo polisi ya Libnan ilisema,jeshi la wanaanga la Israel lilikwishatuma ndege za kijeshi katika anga ya Libnan kinyume na makubaliano ya kuweka chini silaha yaliyofikiwa chini mapema wiki hii.Jeshi la Israel linasema kitendo hicho kimelengwa kuzuwia silaha wanazopatiwa Hisbollah kutoka Iran na Syria.Israel inapanga kuendelea na opereshini hizo hadi vikosi vya kimataifa vitakapotumwa katika eneo hilo.Kundi la mwanzo la wanajeshi 50 wa Ufaransa limeshawasili katika mji wa bandari wa Nakura,kusini mwa Libnan.Na umoja wa mataifa umezitolea mwito nchi za Ulaya ziwajibike zaidi.Wakati huo huo katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan ametoa mwito vizuwizi vya angani na baharini vilivyowekwa dhidi ya Libnan viondoshwe,ili ipatikane njia ya kuwahudumia ipasavyo wananchi.Israel inasema lakini itaendeleza vizuwizi hivyo kwa lengo la kuzuwia Hisbollah wasipatiwe silaha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW