Jeshi la anga la Nigeria lakiri kuhusika na shambulizi
28 Januari 2024Jeshi hilo limesema kuwa Kiongozi wake wa ngazi ya juu Hasan Abubakar alizitembelea jamii zilizoathiriwa na shambulio hilo baada ya kuhakikisha ripoti za mkasa huo.
Aboubakar alisema kuwa mashambulizi hayo hayakufanywa kwa makusudi bali yaliwalenga magaidi na wezi wa mifugo kutokana na ongezeko la ukosefu wa usalama katika eneo hilo kwa wakati huo.
Soma pia: Watu 30 wauawa Nigeria
Itakumbukwa kuwa, mwezi Januari mwaka 2023, makumi ya wafugaji wa kabila la Fulani waliuwawa katikati mwa jimbo la Nasarawa baada ya kushambuliwa kwa mabomu yaliyoporomoshwa kwa njia ya anga.
Soma pia: Watu 113 wauawa katika mashambulizi katikati mwa Nigeria
Jeshi la anga limesema kukutana na wawakilishi wa wahaathiriwa wa shambulio hilo "kutasaidia katika kujibu baadhi ya maswali muhimu, kuboresha uwajibikaji, uwazi" na kuzuia matukio kama hayo katika siku zijazo. Hata hivyo suala la fidia halikutajwa.