1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Colombia lamkomboa Betancourt

Kalyango Siraj3 Julai 2008

Makamando wa Colombia waliwahadaa waasi wa FARC

Raia watatu wa Marekani waliokuwa wanashikiliwa na waasi wa Colombia wa FARC ambao wameokolewa na jeshi la serikali ya Bogota (Kutoka kushoto hadi kulia ) Marc Goncalves, Kein Stabler na Thomas HowesPicha: picture-alliance/dpa

Jeshi la Colombia limewaokoa mateka kadhaa kutoka mikono ya waasi wa mrengo wa kushoto nchini Colombia. Moja wa mateka waliokolewa ameielezea operesheni hiyo kama tukio moja la kihistoria.

Operesheni iimefanyika katika misitu ya nchi hiyo na katika maeneo yanaosimamiwa na waasi hao.

Waliokombolewa ni 15 mkiwemo raia wa Marekani watatu na mwanasiasa mashuhuri Ingrid Betancourt, „Ahsante sana kwa Wakolombia wote,na kwa kila mtu yote duniani aliekuwa nasi.Ahsante kwa nchi yangu na kwa jeshi na operesheni ilikuwa safi. „

Bi Ingrid Betancourt akizungumza mbele ya waandishi habari pamoja na rais wa nchi hiyo Alvaro Uribe punde tu baada ya kuwasili mjini Bogota kutoka mafichoni ambako amekuwa akishikiliwa mateka kwa mda wa miaka sita.

Betancourt ni mwanasiasa wa Colombia ambae ana uraia wa nchi mbili Colombia anakozaliwa na Ufaransa ambako mme wake anakotokea.

Alichukuliwa mateka na waasi wa FARC miaka sita iliopita wakati akitafuta kura za kutaka kuchaguliwa kama kiongozi wa nchi yake.

Akieleza jinsi operesheni ya kuwakomboa ilivyokuwa alisema kuwa mwanzo yeye na wenzake 14 hawakujua kuwa waliokuwa wanawachukua mateka tena hiyo jana walikuwa wanajeshi wa Colombia ambao walijifanya kama watu wengine kabisa.Baadhi yao walikuwa wamevaa T-shirt zilizokuwa na picha ya mwanamapinduzi Che Guevara. Ni hadi pale walipukuwa angani katika Helikopta ndipo walijua ukweli wa mambo, „Mkuu wa operesheni alisema kuwa sisi ni kutoka jeshi la Colombia sas mko huru.Helikopta kidogo ianguke kwa sababu tuliruka,kupiga kelel,tukila na kukumbatiana kwani hatukuweza kuamini.

Mmetupa zawadi ya muujiza.Huu ni muujiza…"

Miongoni mwa waliookolewa ni raia watatu wa Marekani ambao walichukuliwa na waasi hao,baada ya ndege yao kuanguka.Walikuwa katika kikosi cha Marekani kinachopambana dhidi ya madawa ya kulevya.Walikamatwa mwaka wa 2003.

Waziri wa Ulinzi wa Colombia Juan Manuel Santos amesema kuwa operesheni ya kuwakomboa ilikuja baada ya jeshi kufaulu kupenya waasi hao na kuongeza kuwa bila shaka itaingia katika Daftari ya kihistoria.

Mateka waliokolewa bila hata kufyatua risasi yoyote.

Operesheni imekaribishwa duaniani kote.

Waasi wa FARC wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya Colombia kwa kipindi cha miaka 40 na sasa wanaonekana kama nguvu zimewaaishia.

Kulikuwa na hofu ya maisha ya Benatcourt kufuatia kuonekana katika mkanda uliotolewa na waasi hao ukimuonyesha kama mgonjwa sana.Lakini sasa anaonekana mwenye afya.

Raia kadhaa walimiminika katika barabara za mjini Bogota kushangilia kukombolewa kutoka kwa mikono ya waasi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW