1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Guinea lasema Conde yuko nyumbani na mkewe

30 Novemba 2021

Utawala wa kijeshi nchini Guinea umetangaza kuwa rais aliyeondolewa madarakani Alpha Conde amepelekwa nyumbani kwa mkewe katika mji mkuu Conakry.

Guinea Junta
Picha: Sunday Alamba/AP/picture alliance

Utawala huo umefichua pia mahali aliko kiongozi huyo aliyepinduliwa baada ya kumshikilia bila kuwasiliana naye kwa miezi kadhaa.

Conde mwenye umri wa miaka 83, aliiongoza nchi hiyo kwa karibu miaka 11 kabla ya kuondolewa Septemba 5 katika mapinduzi ya kijeshi.

Katika taarifa iliyorushwa na televisheni ya serikali, jeshi limesema Conde sasa yuko nyumbani na mkewe, Hadja Djene Kaba Conde, katika vitongoji vya Conakry.

Haikusema kama Conde yuko chini ya kifungo cha nyumbani au kama anakabiliwa na vizuizi vingine.

Taarifa hiyo aidha imesema serikali ya kijeshi inayojiita National Rally Committee for Development - CNRD, itaendelea kumpa mkuu huyo wa nchi wa zamani heshima anayostahili, na bila shinikizo lolote la kitaifa au kimataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW