1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Iran lakanusha kuwepo kwa mazungumzo na Marekani

25 Machi 2026

Israel na Iran zimeendelea kushambuliana kwa makombora Jumatano wakati jeshi la Iran limekanusha madai ya Rais Donald Trump kuwa Marekani inafanya mazungumzo ya kuvisitisha vita hivyo.

Mwanajeshi wa jeshi la mapinduzi la Iran akishika doria mjini Tehran
Mwanajeshi wa jeshi la mapinduzi la Iran akishika doria mjini TehranPicha: Sobhan Farajvan/Pacific Press/Sipa USA/picture alliance

Jeshi hilo la Iran linasema Marekani iko katika mazungumzo peke yake.

Hatua hiyo ya Kamandi ya Pamoja ya Jeshi la Iran inayodhibitiwa na wakuu wenye misimamo mikali kutoka Jeshi la Mapinduzi kukanusha kuwepo kwa mazungumzo, inakuja wakati ambapo ripoti zinaarifu kuwa Marekani imetoa mpango wa hoja 15 za kujadiliwa katika mazungumzo hayo kwa Tehran.

Uongozi wa Iran awali ulisema kuwa hauwezi kuingia katika majadiliano na Marekani kwa kuwa nchi hiyo iliishambulia mara mbili wakiwa kwenye mazungumzo.

Wakati huo huo, jeshi la Israel limesema limefanya mashambulizi yaliyolenga miundo mbinu kote mjini Tehran.

Kuwait na Saudi Arabia nazo zimesema zimezuia mashambulizi ya droni ingawa hazikutaja zilikotokea droni hizo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW