1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Iran lasema limelenga kambi za kijeshi za Israel

12 Machi 2026

Jeshi la Iran limesema leo kuwa limelenga kambi za kijeshi za Israel pamoja na shirika la usalama wa ndani Shin Bet huku vita kati ya Marekani, Israel na nchi hiyo vikiingia siku ya 13.

Iran Tehran 2026 | Wanajeshi wa Iran
Mkuu wa jeshi la Iran Amir Hatami (katikati) katika picha ya pamoja na maafisa wa jeshi mnamo 7.01.2026 Picha: Iranian Army Media Office/AFP

Katika taarifa kupitia televisheni ya kitaifa, jeshi la Iran limesema kuwa kambi za jeshi la anga za Palmachim na Ovda za utawala wa Kizayuni pamoja na makao makuu ya Shin Bet zililengwa kwa droni.

Wakati huo huo, mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, yameharibu takriban maeneo manne ya kitamaduni na kihistoria, yakiwemo makasri na msikiti wa kale, hali inayoibua wasiwasi kuhusu athari za vita hivyo vinavyopanuka dhidi ya maeneo yanayolindwa ambayo ni muhimu kwa utambulisho wa Iran na historia ya dunia.

Uharibifu huo umezisukuma Iran na Lebanon kutuma ombi wiki hii kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni, UNESCO, kuongeza maeneo zaidi kwenye orodha yake ya ulinzi iliyoimarishwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW