1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Jeshi la Israel ladai kuharibu kamandi ya kijeshi ya Hamas

15 Desemba 2023

Jeshi la Israel limesema leo kwamba limekamata na kuharibu kamandi inayotumiwa na wanamgambo wa kundi la Hamas katika mji wa Gaza.

Israel | Mzinga wa Israel ukifyetua kombora kuelekea Gaza
Jeshi la Israel linaendesha operesheni ya kijeshi Ukanda wa Gaza kwa dhamira ya kulitokomeza kundi la HamasPicha: Leo Correa/AP/picture alliance

Jeshi hilo la IDF limeongeza kuwa, limeharibu handaki moja linalotumiwa na Hamas.

IDF inadai kuwa wanamgambo kadhaa wameuawa wakati wa oparesheni ya kijeshi katika wilaya ya Shejaiya, inayoonekana kama moja ya ngome za mwisho iliyokuwa chini ya Hamas huko Gaza.

Taarifa hizo hata hivyo hazikuweza kuthibitishwa na vyanzo huru.

Kwa upande mwengine, Israel wiki hii imefanya oparesheni kubwa ya kijeshi katika mji wa Ukingo wa Magharibi wa Jenin na kambi yake ya wakimbizi.

Wizara ya afya ya Palestine imesema oparesheni hiyo imedumu takriban siku tatu na kwamba watu 12 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW