1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yadai kuharibu maficho ya wanamgambo wa Hamas Gaza

30 Desemba 2023

Jeshi la Israel limesema limeharibu handaki lililokuwa linatumiwa kama maficho ya kiongozi wa kundi la Hamas huko Gaza, Yehya Sinwar.

Nahostkonflikt - Flüchtlingsviertel Al-Maghasi
Wapalestina wakishuhudia uharibu mkubwa baada ya shambulizi la Israel katika kambi ya wakimbizi ya Al Maghasi huko Deir Al-Balah, GAza: 25.12.2023Picha: Mohammed Talatene/dpa/picture alliance

Inaaminika kuwa Sinwar ndiye aliyepanga shambulio la kigaidi la Hamas mnamo Oktoba 7 ambalo lilisababisha vifo vya watu 1,200 huku wengine 240 wakichukuliwa mateka.

Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant amesema wanajeshi wa Israel wamefanikiwa kuwasili eneo la kamandi la Hamas na kwenye maghala ya silaha.

Hayo yanajiri wakatiIsrael ikiendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza  hasa katika kambi ya Nuseirat na kitongoji cha Khan Younis.

Wakaazi wa eneo hilo wamesema karibu watu 200 wameuawa ndani ya saa 24 zilizopita. Kulingana na Wizara ya Afya huko Gaza inayodhibitiwa na Hamas, mzozo huo tayari umesababisha vifo vya Wapalestina 21,320.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW