1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel lamshikilia mkurugenzi wa hospitali Gaza

28 Desemba 2024

Maafisa wa afya wa Gaza wamesema vikosi vya Israel vimemuweka kizuizini mkurugenzi wa hospitali kaskazini mwa Gaza, ambayo Shirika la Afya Ulimwenguni, lilisema kuwa ilisitishwa kutokana na operesheni za Israel.

Gazastreifen Innenhof des Kamal Adwan Hospital in Beit Lahia nach israelischem Luftangriff
Muonekano wa uharibifu kufuatia shambulio la Israeli kwenye ua wa Hospitali ya Kamal Adwan Desemba 25, 2024. Picha: Khalil Ramzi Alkahlut/Anadolu/picture alliance

Taarifa ya wizara ya afya inayodhibitiwa na kundi la Hamas imeeleza kuwa "vikosi vya Israel vimewachukua makumi ya wahudumu kutoka Hospitali ya Kamal Adwan na kwenda nao kizuizini kwa mahojiano, akiwemo mkurugenzi, Hossam Abu Safiyeh." Kadhalika shirika la ulinzi wa raia wa Gaza liliripoti kuwa Abu Safiyeh yupo kizuzini, na kuongeza kuwa mkurugenzi wa shirika hilo kwa kaskazini, Ahmed Hassan al-Kahlout, ni miongoni mwa wanaoshikiliwa. Jana Ijumaa, jeshi la Israel lilifanya operesheni katika eneo la Hospitali ya Kamal Adwan, kwa madai kuwa kituo hicho ni "ngome muhimu ya makundi ya kigaidi", kauli ambayo imekanushwa na Hamas.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW