1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel laondoka katika vijiji vya kusini, Lebanon

18 Februari 2025

Jeshi la Israel limejiondoa katika vijiji vya kusini mwa Lebanon lakini limesalia katika maeneo matano, huku muda wa mwisho wa kujiondoa kwa jeshi hilo ukifikia kikomo leo.

Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz wakati wa sherehe ya kuachia wadhifa wa waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo mjini Jerusalem mnamo Nivemba 10,2024
Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel KatzPicha: MENAHEM KAHANA/AFP

Waziri wa ulinzi wa Israel Israel Katz, amethibitisha leo kuwa wanajeshi wake wamesalia katika maeneo matano kusini mwa Lebanon baada ya kumalizika kwa muda wa mwisho wa kuondoka nchini humo, huku akiahidi kuchukua hatua dhidi ya ukiukaji wowote wa makubaliano ya amani na kundi hilo la wanamgambo la Hezbollah.

Israel kuchukuwa hatua dhidi ya ukiukaji wowote wa Hezbollah

Katika taarifa, Katz amesema kuwa jeshi hilo la Israel litasalia katika eneo salama na kuwa na udhibiti wa maeneo matano ya kimkakati huku akiongeza kuwa litaendelea kuchukua hatua za nguvu dhidi ya ukiukaji wowote utakaofanywa na Hezbollah.

Lebanon yasema Israel lazima iondoke nchini mwake

Awali, chanzo kimoja cha usalama cha Lebanon, kililiambia shirika la habari la AFP kwamba jeshi la Israel limejiondoa katika vijiji vyote vya mpakani isipokuwa katika maeneo matano.

Wakati huo huo, jeshi la Lebanonlimetangaza kupeleka wanajeshi wake katika vijiji vya mpakani vilipoondoka vikosi vya Israel.

Magari ya kijeshi ya Israel kusini mwa LebanonPicha: Stringer/Anadolu/picture alliance

Miji na vijiji kadhaa vya mpakani, ikiwa ni pamoja na manispaa ya Mais al-Jabal, zilikuwa zimetoa wito kwa wakaazi waliokimbia makazi yao kusubiri hadi jeshi la Lebanon litakapochukuwa udhibiti wa maeneo hayo kabla ya kurejea, ili kuhakikisha usalama wao.

Lebanon: Rais mpya aibua matumaini ya utulivu Mashariki ya Kati

Mamlaka ya Lebanon imekataa kuongezwa tena kwa muda wa kujiondoa kwa vikosi vya Israel na kuwataka wafadhili wa makubaliano hayo kuishinikiza Israel kujiondoa.

Maandamano yafanyika Tel Aviv na Jerusalem

Watu jana walifanya maandamano mjini Tel Aviv na Jerusalem ikiwa imesalia muda wa chini ya wiki mbili kabla ya kukamilika kwa awamu ya sasa ya makubaliano ya amani kwaGaza.Mazungumzo kuhusu awamu ya pili ya mazungumzo hayo ya amani bado haijaanza.

Zaidi ya mateka 70 bado wanashikiliwa Gaza, huku karibu nusu wakihofiwa kuwa wamekufa.

  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW