1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Jeshi la Israel latoa wito mpya wa kuhama Beirut Kusini

13 Novemba 2024

Jeshi la Israel mnamo Jumatano limewaaamuru wakaazi wa sehemu za vitongoji vya kusini mwa Beirut kuondoka.

Israel yatoa onyo kwa wakaazi wa Beirut kusini kuhama
Israel yatoa onyo kwa wakaazi wa Beirut kusini kuhamaPicha: FADEL ITANI/AFP

Hii ni mara ya tatu ambapo Israel imetoa onyo kama hilo katika muda wa saa 24.

Eneo hilo la kusini mwa Beirut limeshambuliwa baada ya jeshi la Israel kutoa amri ya watu kuondoka lilitaja eneo hilo kuwa ni ngome ya kundi la Hezobollah.

Picha za chombo cha habari cha AFP zilionyesha moshi mweusi ukifuka katika eneo hilo baada ya kushambuliwa, takriban saa moja baada ya jeshi la Israel kuwaambia wakaazi katika sehemu za vitongoji vya kusini kuondoka.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW